CHIMBUKO LA URA SACCOS LTD

URA Saccos Ltd ni ushirika wa kuweka akiba na kukopa  ulioanzishwa ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania kwa ajili ya watumishi wake Jeshini pamoja na familia zao. Ushirika huu ulisajiliwa mnamo tarehe 06/09/2006 na kupata namba ya usajili DSM 904. Ushirika huu ulizinduliwa rasmi na mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne Mh. Dr Jakaya Mrisho Kikwete mnamo tarehe 09/09/2006 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar Es Salaam.

 

 URA SACCOS LTD INAONGOZWA NA MAMLAKA ZIFUATAZO:

  1. Sheria ya Vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013
  2. Kanuni ya Vyama vya Ushirika ya mwaka 2015
  3. Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018
  4. Kanuni ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2019
  5. Masharti ya Chama (katiba)
  6. Kanuni za Kudumu za Jeshi la Polisi ( PGO 112 para 3)

 

 WAASISI WA URA URA SACCOS LTD:

URA SACCOS Ltd ilianzishwa kutokana na wazo lililotolewa na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Said Ally Mwema IJP mstaafu kwa kushirikiana na Bodi ya mpito iliyofanya kazi ya kusajili chama na kutafuta wanachama waanzilishi, wajumbe wa Bodi ya mpito ambao walikuwa ni Walfgang R. Gumbo – SACP mstaafu, Elice Angelo Mapunda, Albert Mathias Nyamhanga – SP, Kim Onai Mwenfula – INSP, Sebastian Masinde – SP  Mstaafu, Said Kitinga CPL – X Police, Eliasifu Mlay – mtumishi raia , Edda Hokororo – INSP Marehemu, Benard Samala – INSP .

MLEZI WA URA SACCOS:

Mlezi wa URA SACCOS Ltd ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Madhumuni ya chama

Madhumuni ya chama hiki ni kuinua, kustawisha na kuboresha hali ya wanachama wake katika kukidhi mahitaji mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa kufuata taratibu za kidemokrasia, misingi, kanuni na sheria za vyama vya Ushirika, kanuni ya kudumu ya Jeshi la Polisi PGO (112) iii, Ustawi wa jamii na uchumi.

Jukumu letu

Jukumu letu ni kutoa huduma bora za kifedha kwa masharti nafuu yanayo kidhi mahitaji ya wanachama na wateja.

Lengo Letu

Lengo letu ni kuwa asasi kubwa ya huduma za kifedha iliyoendelevu yenye mtandao wa kifedha na yenye uwezo mkubwa wa kuboresha hali ya ustawi kiuchumi na kijamii kwa watumishi wa Jeshi la Polisi Tanzania na familia zao.