a) Maelekezo sahihi ya namna ya kupiga picha kabla ya kuomba Kitambulisho kwenye mfumo:
- Kamera ya kawaida au ya Simu yenye uwezo angalau wa kuanzia megapixel 2.
- Picha ipigwe kwenye mwanga wa mchana bila flash na kivuli.
- Upigapo picha simama umbali wa futi 1 toka kwenye usuli ( background) nyeupe au bluu.
- Piga picha ukiwa umevaa shati au blauzi ya kiraia.
- Simama wima ukiwa umeangalia camera wakati wa upigaji picha.
- Usifumbe macho wakati wa kupigwa picha.
- Fumba mdomo na usitabasam.
b) Picha zinazokubalika:
- Inaweza kuwa ya kawaida bila kufunika kichwa.
- Waweza kuvaa miwani ila isiwe mieusi inayofunika macho.
- Waweza vaa hijabu au baragashia .
- Usivae kapelo.
c) Muhimu:
Baada ya kupiga picha yako chukua kalamu yako sasa na karatasi nyeupe na uandike sahihi yako vizuri. Kisha ipige picha sahihi hiyo kukiwa na mwanga mzuri.