HISA

  • Hisa huwakilisha sehemu ya umiliki wa Ushirika (wingi wa hisa ndio ukubwa wa umiliki).
  • Mwanahisa anayo haki kwenye mali yoyote ambayo ushirika unamiliki
  • Mwanahisa anahaki ya kupata gawio kutoka kwenye faida kwa kiwango kilichoamriwa kigawiwe na Mkutano mkuu.
  • Mwana hisa anaweza kupata faida kama thamani ya hisa itapanda
  • Mwanahisa ana haki ya kupiga/kupigiwa kura kwenye mkutano mkuu wa chama kulingana na taratatibu za chama

AKIBA

Hii ni michango ambayo mwanachama anajiwekea katika Akaunti yake mara kwa mara kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya baadaye kadri ya uwezo wake,

Mwanachama anaweza kujiwekea michango hii kutoka kwenye mshahara au fedha taslimu isiyopungua shilingi elfu ishirini (20,000) kila mwezi(inaweza kubadilika kulingana na mahitaji ya wakati husika).

  • Mwanachama aliye na mkopo hata ruhusiwa kupunguza akiba zake chini zaidi ya madeni yake chamani.

 

 

FAIDA ZA AKIBA

  • Haina gharama ya uendeshaji kwa Mwanachama
  • Huduma hii humuwezesha mwanachama kufikia lengo sababu Mwanachama huweza kuweka pesa yake kidogo kidogo kwa muda mrefu
  • Humuwezesha mteja kukopa hadi mara tatu ya akiba aliyojiwekea kwa kuzingatia kanuni za mikopo
  • Huduma hii humuwezesha mwanachama kujenga tabia ya kujiwekea akiba mara kwa mara (saving culture)
  • Huduma hii inatoa faida ya 5.5% kwa mwaka kwa kiasi cha akiba kisichopungua laki tano (tshs 500,000/=).

AMANA

Ni mfumo wa kujiwekea pesa kwa ajili ya kukidhi haja mbalimbli wakati wowote

SIFA NA FAIDA ZAKE

Mwanachama anaweza kuchukuwa pesa kutoka kwenye akaunti hii wakati wowote.

  • Mwanachama atapata 5.5% kwa mwaka kwa kiwango cha shilingi laki tano (tshs 500,000/=) zilizopo kwenye akaunti yake.

 

.