CHIMBUKO LA URA SACCOS LTD

URA SACCOS LTD ni Ushirika wa Akiba na Mikopo ulioanzishwa kwa ajili ya watumishi wa Jeshi la Polisi Tanzania pamoja na Familia zao. Ushirika huu ulisajiliwa mnamo tarehe 06 Septemba, 2006, na kupata namba ya usajili DSR 904. Ushirika huu ulizinduliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne Mheshimiwa Dr. Jakaya M.Kikwete mnamo tarehe 09 Septemba, 2006 katika ukumbi wa Diamond Jubilie Dar es salaam.

 

URA SACCOS LTD ni Chama kinachoongozwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya ushirika sheria na. 20 ya mwaka 2003 na mabadiriko yake.

Waasisi wa URA SACCOS LTD:

URA SACCOS LTD ilianzishwa kutokana na wazo lililotolewa na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania SAIDI ALLY MWEMA IJP Mstaafu kwa kushirikiana na Bodi ya mpito iliyofanya kazi ya kusajili chama na kutafuta wanachama waanzilishi, wajumbe wa Bodi ya Mpito walikuwa: Walfgang R. Gumbu – SACP Mstaafu, Elice Angelo Mapunda-SP, Albert Mathias Nyamhanga – SP, Kim Onai Mwemfula – INSP, Sebastian Masinde SP Mstaafu, Saidi Kitinga – CPL – ex Polisi, Eliasifu Mlay – Mtumishi raia, Eddah I. Hokororo – INSP kwa sasa ni marehemu, Bernard Samala – INSP.

  • Mlezi wa URA SACCOS LTD: Mlezi wa URA SACCOS LTD ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Madhumuni ya chama

Madhumuni ya chama hiki ni kuinua, kustawisha na kuboresha hali ya wanachama wake katika kukidhi mahitaji mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa kufuata taratibu za kidemokrasia, misingi, kanuni na sheria za vyama vya Ushirika

Jukumu letu

Jukumu letu: Kutoa huduma bora za kifedha kwa masharti nafuu yanayokidhi mahitaji ya wanachama na wateja.

Lengo Letu

Lengo Letu: Kuwa Asasi ya huduma za kifedha iliyoendelevu yenye mtandao wa kitaifa na yenye uwezo mkubwa wa kuboresha hali ya ustawi kiuchumi na kijamii kwa watumishi wa Jeshi la Polisi na familia zao