MIKOPO:

Mikopo ni miongoni mwa huduma zinazotolewa na URA SACCOS LTD, ili mwanachama aweze kupata huduma hii, ni lazima atimize masharti ya mkopo anaouomba sanjari na ujazaji fomu na viambatanisho vyake. Mikopo yote inayotolewa kwa wanachama hukatiwa bima ya maisha, ambapo ikitokea mwanachama amefariki dunia chama hakitachukua stahiki za marehemu kufidia deni aliloliacha chamani.

Mikopo ya dharura

  • Hii ni mikopo ambayo hutolewa kwa ajili ya kukidhi dharura ya wanachama.
  • Mikopo hii hupewa kipaumbele cha uharaka ili kukidhi mahitaji ya mwombaji.
  • Mkopo huu hautazidi kiasi cha shilingi milioni moja tu (Tshs 1,000,000/=) kwa muda wa marejesho usiozidi miezi 6
  • Mwombaji inabidi aoneshe viambatanisho vya dharura na sio vinginevyo
  • Mikopo ya Elimu (Elimika)
  • Hii ni mikopo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya elimu kwa wakati, mfano ada, sare n.k
  • Mkopo huu muda wake wa marejesho hautazidi miezi 12
  • Mkopaji atatakiwa kuambatanisha mchanganuo wa malipo kutoka taasisi husika pamoja na akaunti ya shule/chuo husika kwa kuwa pesa zitalipwa moja kwa moja kwenye akaunti ya shule/chou.

Mikopo ya Wajasiriamali

  • Hii ni mikopo maalum kwa ajili ya kuendeleza shughuli za miradi ya uzalishaji mali inayotambulika kisheria
  • Kiwango cha mkopo hakitozidi mara tatu ya akiba za mwombaji zilizokaa chamani miezi mitatu
  • Ni fursa ya kuongeza kipato kutokana na shughuli ya uzalishaji mali atakayoifanya mwanachama.
  • Mkopaji atatakiwa kuwasilisha mchanganuo wa mradi husika, ambapo afisa mikopo atakagua mradi huo ili kujiridhisha.
  • Mwombaji atatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni wanachama wa URA SACCOS LTD
  • Kwa mkopaji wa mara ya kwanza kiwango cha mkopo hakitozidi shilingi milioni ishirini (Tshs 20,000,000/=) na mkopo wa pili hautatolewa ndani ya miezi 6 baada ya mkopo wa kwanza kutolewa
  • Muda wa marejesho hautazidi miaka 4
  • Kwa kiwango cha mkopo kinachozidi shilingi 10 milioni, dhamana itahitajika ambapo mwenza (mke au mume) atahitajika ahusishwe kama mali husika ni ya familia

Mkopo wa Uwiano wa Mshahara

  • Ni mkopo wenye masharti nafuu kwa wanachama ambao ni watumishi tu.
  • Kiwango cha mkopo kitategemea mahitaji ya mwanachama na uwezo wake wa kufanya marejesho katika mshahara bila kuathiri sheria za kazi

Wanachama wanaofukuzwa/wanaotoroka kazi wakiwa bado wanadaiwa watafuatiliwa huko walipo ili walipe madeni na ikishindikana basi mafao yao ya mifuko ya hifadhi ya jamii yatazuiliwa wakati hatua za kisheria zinachukuliwa.

Mikopo ya wanafamilia

  • Hii ni mikopo kwa ajili ya mwenza (mume/mke)wa mtumishi wa jeshi la polisi ambaye ni mwanachama wa URA SACCOS LTD na mwenye shughuli inayomletea kipato halali
  • Elimu ya awali juu ya matumizi bora ya mkopo itatolewa kwa mwanachama
  • Ni fursa ya kuongeza kipato ndani ya familia kumudu mahitaji mbalimbali
  • Mkopo hautazidi mara 3 ya akiba ya mwanachama iliyokaa zaidi ya miezi 3 kwenye chama
  • Kiwango cha juu cha mkopo kwa mwanafamilia hakitazidi shilingi milioni kumi tu (Tshs 10,000,000/=)
  • Wadhamini wawili ambao wote ni wanachama wa URA SACCOS LTD akiwemo yule mwenza wa mkopaji.

Pale ambapo afisa mikopo ataona inafaa atashauri uwepo wa dhamana ya mali sanjari na wadhamini wawili.

MIKOPO YA KUJAZILIZIA (LOAN TOP UP)

Mikopo ya kujazilizia (loan top up) ni aina ya mikopo ambayo itahusisha mikopo iliyotolewa na URA SACCOS LTD  pekee.

Hii ni njia ya kumpatia mkopo mwanachama akiwa amebakiza muda mfupi wa marejesho ya mkopo alionao. Kwa kutumia utaratibu huu deni la mkopo halisi (mkopo bila riba ya mbele) litapunguzwa kutoka katika mkopo mpya utakaotolewa.

SIFA ZA KUPATA MKOPO HUU;

  • katika mikopo hii riba ya mbele kwa mikopo inayojaziliziwa haitatozwa.
  • Marejesho ya mkopo unaojazilizwa lazima yawe yamefanyika kwa muda usiopungua miezi sita (6).
  • mkopo husika uwe umebakiza muda wa marejesho wa miezi kumi na mbili (12) au pungufu.
  • wanachama waliochukua mikopo isiyozidi milioni moja (tshs.1,000,000/=) au ambao salio la mikopo yao halizidi milioni moja (tzs.1,000,000/=) na wamefanya marejesho ya mkopo husika kwa muda usiopungua miezi sita,  muda uliosalia kabla ya mkopo husika kumalizika hautaangaliwa.
  • mkopo mpya utatozwa riba na gharama nyinginezo za mkopo.

HUDUMA  ZA KIJAMII

  •  Mkono wa pole kwa mwanachama aliyejeruhiwa vibaya kazini kiasi cha kuhatarisha maisha yake,  hupewa Tsh. 1,000,000/=
  • Mkono wa pole kwa mwanachama aliyepatwa na majanga ya moto, hupewa Tsh. 1,000,000/=
  • Mkono wa pole kwa mwanachama aliyelazwa hospitalini siku 30 mfululizo, hupewa Tsh. 500,000/=
  • Mwanachama/mwenza akifariki atalipwa rambirambi kiasi cha Tsh. 500,000/=
  • Mwanachama aliyefiwa na mtoto chini ya miaka 18 atalipwa rambirambi ya Tsh. 400,000/= Hii inatolewa kwa watoto wanne tu.