- Kwa kuwa imeonesha, haja ya kuongeza mtaji kupitia Akiba, Amana, na ununuzi wa Hisa, Mkutano Mkuu unaazimia elimu iendelee kutolewa kwa wanachama wote
- Kwa kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni muhimu katika upashanaji wa Habari, Mkutano Mkuu unaazimia mitandao ya Kijamii ya chama ikiwepo Tovuti/Website, Instagram, Youtube na Facebook iliyokwisha anzishwa ianze kutumika live (Mubashara) kwa mwaka 2021.
- Kupitia hoja ya ukaguzi wa mkaguzi wa nje kuhusiana na chama kujenga majengo kwenye maeneo ya Jeshi la Polisi, Mkutano Mkuu umeazimia Bodi ya Chama kufanya mashauriano na uongozi wa Jeshi la Polisi ili kushauri kuandaliwa kwa M.o.U kati ya Jeshi la Polisi na URA SACCOS LTD.
- Kwa kuwa limejitokeza hitaji la kujua uhusiano kati ya maendeleo ya Chama na Ustawi wa Mwanachama mmoja mmoja,Mkutano Mkuu unaazimia tafiti za kitaalam zifanyike ili kubainisha ombi hilo.