MAELEKEZO YA NAMNA Y A KUPIGA PICHA YA KITAMBULISHO CHA URA SACCOS.
- KAMERA YA KAWAIDA/ KAMERA YA SIMU YENYE UWEZO ANGALAU KUANZIA 2 MEGAPIXEL
- PICHA IPIGWE KWENYE MWANGA WA MCHANA BILA FLASH NA KIVULI.
- UPIGAPO PICHA SIMAMA UMBALI WA FUTI MOJA TOKA KWENYE USULI [ BACKGROUND].
- PIGA PICHA UKIWA UMEVAA SHATI LA KIRAIA.
- SIMAMA WIMA UKIWA UNAANGALIA KAMERA WAKATI WA UPIGAJI PICHA.
- USIFUMBE MACHO WAKATI UNAPI GWA PICHA.
- FUMBA MDOMO NA USITABASAMU.
PICHA ZINAZOKUBALIKA.
- INAWEZA IKAWA YA KAWAIDA BILA KUFUNIKA KICHWA.
- UNAWEZA KUVAA MIWANI ILA ISIWE MIEUSI INAYO FUNIKA MACHO.
- UNAWEZA KUVAA HIJABU AMA BHAGALISHIA.
- USIVAE KAPELO.
MUHIMU: BAADA YA KUPIGA PICHA YAKO CHUKUA KALAMU NA KARATASI NYEUPE NA UANDIKE SAHIHI YAKO ,KISHA IPIGE PICHA SAHIHI YAKO KUKIWA NA MWANGA MZURI.
Baada ya kupiga picha na sahihi yako ingia kwenye tovuti ya URA SACCOS ambayo ni www.urasacoss.co.tz, jaza fomu ya maombi ya kitambulisho ambatanisha picha na sahihi yako.AMA BONYEZA LINK HII HAPA CHINI KUIPATA FOMU NA UANZE KUJAZA.