- Kwa malengo ya kulinda na kuongeza ukwasi wa chama Mkutano Mkuu umeazimia yafuatayo: –
- Kuongeza kiwango cha kiingilio cha mwanachama mpya kutoka Tshs. 10,000/- na kuwa 20,000/-
- Sehemu ya malipo ya Posho ya Kujikumu Vikao kwa wanachama iwekwe kwenye akaunti zao za Amana ili waweze kupata huduma za URA MOBILE.
- Kulingana na takwa la kisheria Mkutano Mkuu umeazimia Riba ya Mkopo kushuka kutoka 7.5% na kuwa 6.6% kwa njia ya Mnyoofu (Straight Line Balance Method) sawa na 12% kwa njia ya Salio Linalopungua (Reducing Balance Method).
- Kutokana na uboreshaji wa huduma kwa wanachama Mkutano Mkuu umeazimia kuelimisha na kuhamasisha wanachama namna ya matumizi sahihi ya Mfumo wa Kidijitali wa URA MOBILE MONEY ili kurahisisha huduma kwa wanachama.
- Katika kufanya tathmini za kina za chama, Mkutano Mkuu umeazimia kufanya utafiti wa ufanisi wa bidhaa zitolewazo kwa wanachama wa URA SACCOS LTD ikiwa ni pamoja na kuangalia bidhaa na huduma mpya zitakazo wanufaisha wanachama.
- Katika utoaji elimu Mkutano Mkuu umeazimia yafuatayo: –
- Elimu juu ya kuongeza viwango vya uwekaji wa Akiba, Hisa na Amana ikiwa ni pamoja na uhamasishaji kwa wanachama iendelee kutolewa.
- Elimu kwa Wawakilishi na Watendaji zitolewe kikanda.
- Kwa kuwa mikopo ya taslimu imekuwa na changamoto kubwa ya marejesho na ili kupunguza idadi ya Mikopo chechefu, Mkutano Mkuu umeazimia yafuatayo:-
- Mwakilishi wa mkopaji husika kufuatilia marejesho kwa wakati kwa kumkumbusha mara kwa mara mkopaji.
- Mdhamini wa mkopaji ajaze fomu maalum ya kisheria na kutoa ridhaa ya kubeba deni pindi mkopaji atakaposhindwa kurejesha mkopo huo.