Mkutano Mkuu wa 15 wa URA SACCOS umetamatika tarehe 20/10/2023 mkoani Morogoro ukiongozwa na kauli mbiu isemayo ”Hatimaye Tumefika, Huduma za URA Saccos Ltd Kiganjani”. Mgeni rasmi kwenye Mkutano huo alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini afande IGP Camillus Wambura ambaye alisema kuwa “Ambao bado hawajajiunga katika Chama hiki wajiunge ili wafaidike na huduma zinazotolewa na URA SACCOS na ni vyema mkafanya utafiti kujua ni huduma gani ambazo mnaweza kuziboresha ili ziwafikie Wateja wa Chama hiki”
Aidha wajumbe wa mkutano huo wamefanya uchaguzi wa viongozi wa Bodi ya chama pamoja na Kamati ya usimamizi ambapo wamemchagua Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu CP – Suzan Kaganda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama na Kamishna wa Polisi Jamii CP – Faustine Shilogile kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi.
Wajumbe Wengine wa Bodi Waliochaguliwa ni: –
1. SACP David Misime
2. ACP Edda Mkisi
3. ACP Mussa Ali Mussa
4. ASP Sweetbert Gonda
5. INSP Gilbert Chuwa
6. A/INSP Christopher Mwambona
7. CPA Neema Haule
Kamati ya Usimamizi waliochaguliwa ni: –
- SP – Juma Kanena (Mwenyekiti),
- INSP – Pieritha Gachinya (Mjumbe) na
- CPA Amiri Mgori – A/INSP (Makamu Mwenyekiti).