
Mwenyekiti wa bodi ya URA SACCOS LTD yupo kwenye ziara ya kutembelea matawi ya URA SACCOS LTD kuona namna yanavyotoa huduma kwa wanachama wake pamoja na kubaini changamoto zilizopo kwenye matawi hayo. Aidha kupitia ziara hiyo, Mh. Balozi Kaganda amepata wasaa wa kuzungumza na wanachama wa URA SACCOS na kuendelea kuwapa elimu ya ushirika hususani katika uwekaji wa AKIBA, AMANA na HISA pamoja na matumizi sahihi ya fedha.

Ziara hiyo ndani ya mkoa wa Kigoma ilifanyika kuanzia tarehe 23/01/2025 hadi 24/01/2025 kwa kutembelea ofisi za tawi hilo na kufanya kikao na wanachama. Tarehe 26/01/2025 hadi 27/01/2025 alifanikiwa kutembelea tawi la Mwanza na kufanya kikao na wanachama wa mkoa huo.
Kadhalika ziara hiyo katika mikoa tajwa imekuwa yenye manufaa makubwa kwa wanachama na chama kwani imeongeza hamasa, tija na hari kwa watendaji na wanachama kiujumla kuendelea kuongeza akiba zao ndani ya chama na kuendelea kukiamini chama.
Mwenyekiti wa bodi Balozi Kaganda – CP anaendelea na ziara yake kwenye matawi yote ya URA SACCOS LTD nakuzungumza na wanachama kwenye mikoa atakayotembelea.
https://www.instagram.com/p/DFX4QFRMkX1/?igsh=MTNkZzkzMDNnZ2ZibA==