Huduma za chama, popote ulipo
Ingia kwenye akaunti yako ya mwanachama kuomba mkopo, kitambulisho na huduma nyingine; tumia URA Mobile kwa salio, akiba, hisa na amana; na omba mkopo wa mshahara kupitia ESS.
URA Mobile
URA Mobile ni huduma ya chama kwenye simu yako. Inakuwezesha kuweka akiba, hisa na amana, kuangalia salio na kutoa amana bila kufika tawini.
USSD: piga *149*32#
Ingiza PIN yako, kisha chagua huduma:
- 1Angalia salio
- 2Miamala 5 ya mwisho
- 3Taarifa ya akaunti
- 4Omba mkopo
- 5Weka fedha (akiba, hisa au amana)
- 6Toa fedha (kutoka amana)
- 7Lipa mkopo
- 8Akaunti yangu (k.m. kubadili PIN)
App ya Android
- Ingia Play Store, tafuta "Ura Saccos" na ubonyeze Install.
- Fungua App ya URA Mobile, ingiza namba yako ya simu ikianza na 255, kisha PIN uliyotumiwa.
- Subiri uidhinishwe. Baada ya hapo utahitaji PIN tu kuingia.
Kuweka na kutoa fedha ni kuhamisha kati ya akaunti yako ya chama na Tigo Pesa au Airtel Money; utathibitisha kwa PIN ya mtandao wako na kupokea SMS.
Kujiunga
Jaza fomu ya kujiunga na URA Mobile na uiwasilishe tawini. Fomu hiyo hiyo hutumika kubadili namba ya simu, ukipoteza simu, au ukisahau PIN.
Fomu na mwongozo wa URA Mobile

Mkopo wa mshahara kupitia ESS
Kuanzia Januari 2026, mkopo wa uwiano wa mshahara hutolewa kupitia mfumo wa ESS (e-Watumishi) wa maombi ya mikopo kwa watumishi wa umma, kwa uamuzi wa Mkutano Mkuu wa 17.
- 1
Jisajili na uingie
Jisajili kwenye mfumo wa e-Watumishi (ESS), kisha ingia kwa namba yako ya utumishi (check number) na nywila.
- 2
Chagua URA SACCOS
Fungua moduli ya E-Mkopo, angalia katalogi ya mikopo, na uchague "URA SACCOS SALARY LOAN".
- 3
Kokotoa mkopo wako
Tumia kikokotoo kuona kiwango cha juu unachostahili, au weka kiasi, muda wa marejesho au makato ya kila mwezi unayotaka. Muda hufuata mkataba wako au umri wa kustaafu.
- 4
Tuma maombi
Jaza anwani, sababu ya mkopo, namba ya akaunti na tawi la URA SACCOS, hifadhi, kisha tuma kwa namba ya uthibitisho (OTP) itakayotumwa kwenye simu iliyosajiliwa kwenye e-Watumishi.
- 5
Ofa na malipo
URA SACCOS hupokea na kuhakiki maombi na kutoa ofa; unaikubali, mwajiri anapitisha, na mkopo unatolewa. Makato huondolewa mkopo ukimalizika.
Mikopo ya biashara na ya dharura bado huombwa ofisini au kupitia WhatsApp. Mikopo yote na masharti yake
Omba kitambulisho cha uanachama
Omba kitambulisho kupitia akaunti yako ya mwanachama (member portal). Picha yako iwe kama ifuatavyo:
- Kamera ya kawaida au ya simu yenye angalau megapixel 2
- Mwanga wa mchana, bila flash wala kivuli
- Simama futi moja mbele ya ukuta mweupe au wa bluu
- Vaa shati au blauzi ya kiraia
- Simama wima ukiangalia kamera; usifumbe macho; fumba mdomo bila kutabasamu
- Picha ya kawaida bila kufunika kichwa; hijabu au baraghashia zinaruhusiwa, kapelo hapana
- Miwani inaruhusiwa, isipokuwa miwani myeusi inayoficha macho
Kisha andika sahihi yako kwenye karatasi nyeupe na uipige picha kwenye mwanga mzuri.
Kuwasilisha
Wasilisha picha na sahihi yako tawini au kwa mwakilishi wako. Watasasisha wasifu wako kwenye mfumo wa uanachama (membership portal).
