Maswali ya mara kwa mara
Majibu mafupi kuhusu uanachama, mikopo na akiba. Kama swali lako halipo, tuandikie.
Uanachama
- Askari na watumishi wa Jeshi la Polisi Tanzania. Jaza fomu ya uanachama ofisini au anza kupitia ukurasa wa Jiunge Nasi; makato ya akiba ya kila mwezi huanza kwenye mshahara wako.
Mikopo
- Mkopo wa biashara ni hadi mara tatu ya jumla ya akiba yako, kwa miezi 12 hadi 48. Mkopo wa dharura ni hadi TZS 1,000,000 kwa miezi 1 hadi 12. Mkopo wa mshahara unategemea kanuni ya theluthi mbili: makato yote hayawezi kuzidi 2/3 ya mshahara wako wa msingi.
- Asilimia 12 kwa mwaka kwa salio linalopungua, kwa aina zote tatu za mikopo. Kuna ada ya uchakataji ya 1% na bima ya 1% kwa mwaka ya kiasi cha mkopo.
- Ingia kwenye akaunti yako ya mwanachama (member portal) na uombe mkopo wa biashara au wa dharura mtandaoni, au omba tawini. Mkopo wa mshahara na nyongeza yake huombwa kupitia mfumo wa ESS wa mwajiri.
- Kila akaunti ya mwanachama ina control number. Lipa kwa benki au kwa simu ukitumia control number hiyo; malipo yanaonekana kwenye akaunti yako moja kwa moja. Mkopo wa mshahara hurejeshwa kwa makato ya mshahara.
- Sheria ya Ushirika inaruhusu mkopo wa hadi miaka mitano; chama kinatoa hadi miaka minne. Mikopo hutokana kwa kiasi kikubwa na michango ya wanachama, kwa hiyo kuongeza muda kungeongeza pia kiasi cha kukopa; bila kuongeza michango, chama kingeweza kushindwa kutoa huduma kwa wakati. Muda unaweza kuongezwa kama ukwasi wa chama utaruhusu.
Akiba
- Kupitia URA Mobile: piga *149*32# na uchague Angalia salio au Taarifa ya akaunti, au tumia App. Pia unaweza kuuliza tawini au ofisini; taarifa kamili ya akaunti inaweza kutumwa kwa barua pepe yako.
- Ndiyo. Jaza fomu tawini au ofisini, au wasiliana na mwakilishi wako; mabadiliko yanaanza mwezi unaofuata wa mshahara.
- Akiba ndiyo msingi wa mikopo ya chama, na mara nyingi mkopo wa mwanachama ni mkubwa kuliko akiba yake, kwa hiyo sehemu ya mkopo huo ni akiba za wanachama wenzake. Ili kuchukua akiba yako, rejesha kwanza mkopo. Hata hivyo unaweza kuomba kiasi cha akiba kinachozidi deni lako la mkopo.
- Sheria ya Vyama vya Ushirika hairuhusu mwanachama kuchukua sehemu ya akiba yake, lakini chama kinaruhusu kuchukua hadi asilimia 40 ya akiba ya msingi, ukibakiza asilimia 60. Toa notisi ya angalau siku 90, kwa sababu fedha hizo ziko kwenye mzunguko wa mikopo ya wanachama.
- Gawio ni sehemu ya ziada inayobaki baada ya hesabu za chama kukaguliwa na mkaguzi wa nje na kutoa matengo yote ya kisheria. Mkutano Mkuu huamua gawio, na hugawanywa kulingana na hisa za kila mwanachama. Chama huliweka gawio kwenye akaunti ya hisa ya kila mwanachama kila mwaka wa fedha. Riba juu ya akiba huwekwa moja kwa moja kwenye akiba yako, kwa kiwango kinachoamuliwa na Mkutano Mkuu.
Huduma za simu
- URA Mobile ni huduma ya chama kwenye simu: piga *149*32# (USSD) au tumia App ya URA Mobile kutoka Play Store kuangalia salio, kuweka akiba, hisa na amana, na kutoa amana kupitia Tigo Pesa au Airtel Money. Kujiunga, jaza fomu ya kujiunga na URA Mobile (ukurasa wa Pakua) na uiwasilishe tawini.
Jumla
- Kila mwanachama ana haki sawa na kila mwanachama mwingine, na ana haki ya kutoa maoni yake kwenye vikao vya wanachama ngazi ya wilaya, mkoa na Mkutano Mkuu. Kila wilaya ina mwakilishi anayechaguliwa na wanachama wa wilaya hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya 2013; mwakilishi huyo huwasilisha maoni ya wanachama wake kwenye Mkutano Mkuu, ambao ndio huamua mambo kama viwango vya akiba ya kila mwezi.
- Mahitaji ya mikopo ni makubwa kuliko fedha zilizopo chamani, kwa hiyo posho huwekwa kwenye hisa na amana zako badala ya kulipwa taslimu. Fedha hizo zinabaki kwenye mzunguko wa huduma kwa wanachama, na wewe unapata faida juu ya akiba na gawio juu ya hisa zako; ni uwekezaji wako.
Hukupata jibu? Tuandikie.
