Jiunge nasi
Uanachama ni kwa askari na watumishi wa Jeshi la Polisi Tanzania na familia zao. Pakua fomu, ijaze, kisha iwasilishe tawini au kwa mwakilishi wako.
- 1
Pakua fomu
Pakua fomu ya maombi ya uanachama hapa, au ichukue tawini.
- 2
Ijaze na uiwasilishe
Jaza fomu na uiwasilishe tawini au kwa mwakilishi wako, ukilipa kiingilio. Akiba ya kila mwezi huanza kukatwa kwenye mshahara unaofuata.
- 3
Pata akaunti yako
Unapata akaunti ya mwanachama: ingia kwenye member portal kuomba mkopo, kitambulisho na huduma nyingine; salio na taarifa pia kupitia URA Mobile au tawini.
Unachopata kama mwanachama
- Mikopo kwa riba 12% kwa mwaka, kwa salio linalopungua
- Mkopo wa biashara hadi mara tatu ya akiba yako
- Mkopo wa dharura hadi TZS 1,000,000 bila kipimo cha akiba
- Mkopo wa mshahara unaorejeshwa kwa makato ya mshahara (ESS)
- Hisa na gawio kadri ushirika unavyopata ziada
- Malipo kwa control number, benki au simu
Sifa za kuwa mwanachama
- Awe askari Polisi au mtumishi raia wa Jeshi la Polisi Tanzania, au sehemu ya familia ya mtumishi wa Jeshi la Polisi
- Ajaze fomu ya maombi ya uanachama na kulipa kiingilio
- Akubali kuchangia akiba kila mwezi, kwa kiwango cha chini kilichowekwa na Mkutano Mkuu
- Anunue hisa za chama kwa kiwango kilichowekwa
- Akubali kufuata Sheria ya Vyama vya Ushirika, pamoja na masharti na sera za URA SACCOS LTD
Viwango vya kiingilio, akiba na hisa hutolewa ofisini au kwa barua pepe info@urasaccos.co.tz.
Huduma za kijamii
Chama humfariji na kumsaidia mwanachama katika nyakati ngumu:
- Rambirambi kwa msiba wa mwanachama, mwenza au mtoto
- Pole ya kulazwa kitandani kwa ugonjwa kwa siku 30 au zaidi
- Pole ya kuumia vibaya kazini kiasi cha kuhatarisha maisha
- Pole ya kujeruhiwa kwa risasi
- Pole ya majanga kama moto, mafuriko, tetemeko au upepo mkali
Fomu ya uanachama
Pakua fomu, ijaze kwa ukamilifu, kisha iwasilishe tawini au kwa mwakilishi wako wa wilaya. Watakusaidia kukamilisha usajili wako.
Fomu ya uanachama inapatikana pia tawini.
