Akiba na hisa
Akiba yako ya kila mwezi hukatwa moja kwa moja kwenye mshahara wako. Ndiyo msingi wa uwezo wako wa kukopa, na hisa zako hulipwa gawio.
01
Akiba ya Kila Mwezi
Mchango wako wa kila mwezi unakatwa moja kwa moja kwenye mshahara (kanuni ya makato 667) na kuongeza uwezo wako wa kukopa.
- Makato ya moja kwa moja kwenye mshahara — hakuna kusahau
- Akiba ndiyo msingi wa mkopo: unaweza kukopa hadi mara 3 ya akiba yako
- Unaweza kubadilisha kiasi cha mchango wako (fomu tawini au kupitia mwakilishi wako)
02
Hisa
Umiliki wako katika ushirika. Hisa hununuliwa mara moja au kwa awamu na hulipwa gawio kadri ushirika unavyopata ziada.
- Kila mwanachama anamiliki hisa katika ushirika
- Gawio kulingana na uamuzi wa Mkutano Mkuu
- Angalia hisa zako kwa URA Mobile (*149*32#)
03
Amana
Weka fedha za ziada kwa hiari juu ya akiba yako ya kila mwezi, kwa control number ya akaunti yako.
- Malipo kwa control number — benki au simu
- Taarifa ya akaunti kwa URA Mobile au barua pepe
Weka akiba, hisa na amana, angalia salio na toa amana kwa simu ukitumia URA Mobile (*149*32#). Jinsi ya kutumia URA Mobile
Unaweza kubadilisha kiasi cha akiba yako ya kila mwezi wakati wowote; mabadiliko huanza mwezi unaofuata wa mshahara. Amana za ziada hulipwa kwa control number ya akaunti yako. info@urasaccos.co.tz
