Habari zote

HAFLA

URA SACCOS mshindi kati ya SACCOS za majeshi ya ulinzi na usalama; cheti chatolewa na Gavana wa BoT

Gavana wa Benki Kuu, Bw. Emmanuel Tutuba, amekabidhi cheti kwenye uzinduzi wa taarifa ya utendaji wa SACCOS Tanzania jijini Mwanza.

URASACCOS Admin

Kutokana na utendaji mzuri, URA SACCOS imeibuka mshindi katika SACCOS za majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania na kukabidhiwa cheti na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel M. Tutuba.

Cheti hicho kimetolewa katika hafla ya uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) Tanzania iliyofanyika tarehe 22 Septemba 2023 jijini Mwanza. Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) ndiyo waandaaji wa hafla hiyo iliyotoa tathmini ya utendaji wa vyama kwa mwaka 2022.

Cheti kilipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya URA SACCOS Ltd, CP Benedict M. Wakulyamba.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
URA SACCOS mshindi kati ya SACCOS za majeshi ya ulinzi na usalama; cheti chatolewa na Gavana wa BoT | URASACCOS