Habari zote

MIKUTANO

URA SACCOS yashiriki Kongamano la SACCA 2026 kwa ujumbe wa watu 62

Kongamano la vyama vya ushirika wa akiba na mikopo Afrika limefanyika Dar es Salaam tarehe 11 hadi 16 Oktoba 2026, likishirikisha mataifa zaidi ya 25.

URASACCOS Admin

URA SACCOS Ltd inashiriki Kongamano la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika (2026 SACCA Congress) linalofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 11 hadi 16 Oktoba 2026. Uzinduzi rasmi ulifanyika Jumanne, tarehe 13 Oktoba, kwenye ukumbi wa SuperDome, Masaki, mgeni rasmi akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Gerald Mweli.

Washiriki kutoka mataifa zaidi ya 25 ya Afrika wanashiriki kongamano hili. URA SACCOS Ltd inawakilishwa na ujumbe wa watu 62 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Kamishna wa Polisi Tatu Rashid Jumbe.

Wajumbe wa URA SACCOS wamefuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizotolewa kwenye ukumbi wa JNICC, zikilenga mabadiliko ya kidijitali na mustakabali wa ushirika wa akiba na mikopo barani Afrika.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
URA SACCOS yashiriki Kongamano la SACCA 2026 kwa ujumbe wa watu 62 | URASACCOS