Habari zote

MIKUTANO

Maazimio ya Mkutano Mkuu wa 17 uliofanyika Arusha, 28 Novemba 2025

Akiba ya lazima imeongezwa, riba juu ya akiba na amana imepanda, na mkopo wa uwiano wa mshahara unatolewa kupitia mfumo wa ESS kuanzia Januari 2026.

URASACCOS Admin

Mkutano Mkuu wa 17 wa URA SACCOS ulifanyika tarehe 28 Novemba 2025 jijini Arusha na kuazimia yafuatayo:

  • Kukabiliana na changamoto ya ukwasi kwa kuongeza akiba ya lazima ya kila mwezi: kutoka TZS 30,000 hadi TZS 50,000 kwa mwanachama wa kawaida; TZS 100,000 kwa wawakilishi; TZS 150,000 kwa menejimenti ya makao makuu na matawi; na TZS 200,000 kwa wajumbe wa Bodi na Kamati ya Usimamizi.
  • Kuhamasisha uwekaji wa akiba na amana kwa kupandisha riba: akiba kutoka 5% hadi 8%, na amana kutoka 5% hadi 9%.
  • Elimu ya kikanda kwa wawakilishi iendelee kati ya Februari na Machi 2026, ili wawakilishi watoe elimu iliyo sawa kwa wanachama.
  • Posho ya kikao cha elimu kwa wanachama iongezeke kutoka TZS 60,000 hadi TZS 70,000, na iwekwe kwenye akaunti za wanachama: TZS 50,000 kwenye hisa na TZS 20,000 kwenye amana.
  • Kuimarisha mtaji kwa kuhamisha TZS bilioni 1 kutoka mfuko wa kinga ya ndani ya mikopo kwenda limbikizo la ziada, na gawio la wanachama liwekwe kwenye akaunti zao za hisa.
  • Kutumia TZS bilioni 1 kutoka mfuko wa kinga wa ndani na maendeleo kwa awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la ofisi ya chama.
  • Kuanzia Januari 2026, mkopo wa uwiano wa mshahara utolewe kupitia mfumo wa ESS wa maombi ya mikopo kwa watumishi wa umma.

Nakala kamili ya maazimio inapatikana kwenye ukurasa wa Pakua.

Shiriki: