MIKUTANO
Bodi na menejimenti wapata mafunzo Nairobi na kuahidi kuboresha huduma kwa wateja
Ziara ya mafunzo kwa Kenya National Police DT SACCO imelenga kuongeza weledi katika kuwainua kiuchumi watumishi wa Jeshi la Polisi na familia zao.
URASACCOS Admin
Katika kuhakikisha chama kinaendelea kujiimarisha katika kila sekta, wajumbe wa Bodi, Kamati ya Usimamizi na Menejimenti ya chama wamefanya ziara ya mafunzo jijini Nairobi. Lengo lilikuwa kuongeza weledi katika namna bora ya kuwainua kiuchumi watumishi wa Jeshi la Polisi pamoja na familia zao.
Akizungumza Nairobi, Mwenyekiti wa Bodi, CP Suzan Kaganda, alisema wamejifunza mambo mengi yenye tija katika uendeshaji wa SACCOS na kuweka wazi kuwa wanakwenda kuboresha huduma baada ya mafunzo hayo. Aliipongeza SACCO ya Polisi nchini Kenya kwa viwango bora vya huduma kupitia TEHAMA na kuwa miongoni mwa SACCO bora barani Afrika.
Naye Bw. David Kagogo, Naibu Mwenyekiti wa Kenya National Police DT SACCO, aliwashukuru wajumbe kutoka URA SACCOS kwa kufika kujifunza na kuwaomba kuyachukua mafunzo hayo kikamilifu ili kuongeza ufanisi ndani ya SACCOS ya Polisi Tanzania.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

