Habari zote

HAFLA

CP Tatu Rashid Jumbe apokea uenyekiti wa Bodi kutoka kwa Balozi CP Suzan Kaganda

Makabidhiano yamefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma tarehe 30 Desemba 2025 baada ya CP Kaganda kuteuliwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

URASACCOS Admin

URA SACCOS imekamilisha taratibu za makabidhiano ya uenyekiti wa Bodi tarehe 30 Desemba 2025, ambapo mwenyekiti mstaafu, Balozi CP Suzan S. Kaganda, amemkabidhi CP Tatu Rashid Jumbe, aliyechaguliwa kuwa mjumbe na mwenyekiti wa Bodi ya chama tarehe 28 Novemba 2025.

Balozi Kaganda aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, hivyo akajiuzulu nafasi ya ujumbe wa bodi na uenyekiti aliodumu nao tangu mwaka 2023. Ameshukuru ushirikiano mkubwa wa Mlezi wa Chama, IGP Camillus M. Wambura, wakati akitekeleza majukumu yake kwa lengo la kuboresha ustawi wa watumishi wa Jeshi la Polisi na familia zao.

CP Tatu ameahidi kuendeleza maono na mafanikio yaliyopatikana tangu chama kilipoanzishwa mwaka 2006, na kushirikiana na Bodi, watendaji na wanachama kuiboresha zaidi URA SACCOS. Akiwa Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, ndiye msimamizi mkuu wa ustawi wa watumishi katika Jeshi.

Makabidhiano hayo yamefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Dodoma, na kushuhudiwa na Afisa Ushirika Bw. Haidar Abdulkhakim.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
CP Tatu Rashid Jumbe apokea uenyekiti wa Bodi kutoka kwa Balozi CP Suzan Kaganda | URASACCOS