TAARIFA
URA SACCOS yaingia makubaliano na ALAF: mabati kwa bei nafuu kwa wanachama
Kupitia makubaliano yaliyosainiwa tarehe 3 Septemba 2024, wanachama wanaweza kupata mabati bora ya ALAF kwa bei rafiki kupitia chama chao.
URASACCOS Admin
Tarehe 3 Septemba 2024 URA SACCOS Ltd imeingia makubaliano na kampuni ya mabati ya ALAF, ambapo kupitia makubaliano hayo wanachama wanaweza kupata mabati kwa bei nafuu kupitia chama chao.
Mkataba umesainiwa na Meneja Mkuu wa URA SACCOS Ltd, ACP Kim O. Mwemfula, ukishuhudiwa na mjumbe wa Bodi A/INSP Christopher Mwambona pamoja na watendaji. Kwa upande wa ALAF wamesaini Bw. Satesh Yamsani, Mkuu wa Kitengo cha Biashara, na Bi. Isamba Kasaka, Afisa Masoko, na kushuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Ashish Mistry.
ACP Mwemfula amesema ubia huo utakuwa mkombozi kwa wanachama kwa kuwapatia bidhaa bora kutoka ALAF kwa bei rafiki, kama lilivyo lengo kuu la chama la kuhakikisha wanachama wananufaika kiuchumi. Kwa upande wa ALAF, Bi. Kasaka amesema wanajivunia kuwapa askari mabati bora na imara, kuboresha paa za nyumba zao na kuwapa utulivu kazini.
Kwa kuanzia huduma hizi zinapatikana kwenye matawi ya ALAF yaliyopo mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Arusha na Iringa.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

