Habari zote
MIKUTANO
Mkutano Mkuu wa 12 wafanyika Tanga, 12 Desemba 2020
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhani Kailima, alifungua mkutano uliohudhuriwa na viongozi wa matawi kutoka nchi nzima.
URASACCOS Admin
Mkutano Mkuu wa 12 wa URA SACCOS ulifanyika tarehe 12 Desemba 2020 jijini Tanga na kufunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima. Ulihudhuriwa na viongozi wa matawi ya chama kutoka nchi nzima, pamoja na Mwenyekiti wa Bodi CP Benedict M. Wakulyamba na Meneja Mkuu SSP Kim Onai Mwemfula. Kabla ya mkutano, watendaji wa chama walikuwa na kikao kazi cha siku tatu mkoani humo cha kujengewa uwezo wa kiutendaji.
Mkutano Mkuu uliazimia yafuatayo:
- Elimu iendelee kutolewa kwa wanachama wote ili kuongeza mtaji kupitia akiba, amana na ununuzi wa hisa.
- Mitandao ya kijamii ya chama iliyokwisha anzishwa (tovuti, Instagram, YouTube na Facebook) ianze kutumika mubashara mwaka 2021.
- Kufuatia hoja ya mkaguzi wa nje kuhusu chama kujenga majengo kwenye maeneo ya Jeshi la Polisi, Bodi ifanye mashauriano na uongozi wa Jeshi ili kuandaa makubaliano (MoU) kati ya Jeshi la Polisi na URA SACCOS LTD.
- Zifanyike tafiti za kitaalamu kubainisha uhusiano kati ya maendeleo ya chama na ustawi wa mwanachama mmoja mmoja.
