Habari zote

MIKUTANO

Mkutano Mkuu wa 15 wahitimishwa Morogoro; Bodi mpya yachaguliwa

Wajumbe wamemchagua CP Suzan Kaganda kuwa Mwenyekiti wa Bodi na CP Faustine Shilogile Makamu Mwenyekiti, pamoja na wajumbe wengine wa Bodi na Kamati ya Usimamizi.

URASACCOS Admin

Mkutano Mkuu wa 15 wa URA SACCOS umetamatika tarehe 20 Oktoba 2023 mkoani Morogoro. Wajumbe wa mkutano huo wamefanya uchaguzi wa viongozi wa Bodi pamoja na Kamati ya Usimamizi, ambapo wamemchagua Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Suzan Kaganda, kuwa Mwenyekiti wa Bodi, na Kamishna wa Polisi Jamii, CP Faustine Shilogile, kuwa Makamu Mwenyekiti.

Wajumbe wengine wa Bodi waliochaguliwa ni:

  • SACP David Misime
  • ACP Edda Mkisi
  • ACP Mussa Ali Mussa
  • ASP Sweetbert Gonda
  • INSP Gilbert Chuwa
  • A/INSP Christopher Mwambona
  • CPA Neema Haule

Kamati ya Usimamizi iliyochaguliwa ni SP Juma Kanena, INSP Pieritha Gachinya na A/INSP Amiri Mgori.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
Mkutano Mkuu wa 15 wahitimishwa Morogoro; Bodi mpya yachaguliwa | URASACCOS