HAFLA
URA SACCOS yakabidhi vifaa tiba vya zaidi ya TZS milioni 170 kwa Hospitali ya Polisi Kilwa Road
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, DCP Anthony Rutashuburugukwa, alipokea vifaa hivyo kwa ajili ya hospitali za Polisi.
URASACCOS Admin
URA SACCOS imekabidhi vifaa vya kitabibu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170 kwa ajili ya hospitali za Jeshi la Polisi Tanzania. Makabidhiano yalifanyika katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road, Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Anthony Rutashuburugukwa, alikata utepe kuashiria kupokea vifaa hivyo, akiwa pamoja na mwakilishi wa Bodi ya URA SACCOS, Stanford Busumbiro, na Kamanda wa Kikosi cha Afya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hussein Yahaya.
Baada ya makabidhiano DCP Rutashuburugukwa alikagua vifaa hivyo na kupata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa maabara wa hospitali hiyo.
