Habari zote

TAARIFA

URA SACCOS yaongoza kitaifa katika taarifa ya utendaji wa SACCOS ya TCDC

Taarifa ya mwaka 2025 iliyozinduliwa na Waziri Mkuu inaonesha URA SACCOS inaongoza kwa akiba na amana, rasilimali, bakaa ya mikopo na mtaji.

URASACCOS Admin

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amezindua taarifa ya utendaji wa SACCOS nchini. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam tarehe 15 Oktoba 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), ambapo Kongamano la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika (SACCA) linaendelea.

Taarifa hiyo imeandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini (TCDC) na inaonesha URA SACCOS inaongoza katika maeneo mengi, ikiwemo wingi wa akiba na amana, rasilimali (assets), bakaa ya mikopo na mtaji.

Taarifa hii hutolewa kila mwaka kwa kuzingatia hesabu zilizokaguliwa na kuthibitishwa na wakaguzi wa nje. Jedwali lililotolewa kwenye taarifa hiyo linaonesha ukubwa wa rasilimali za vyama vya ushirika wa akiba na mikopo kwa mwaka 2025.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
URA SACCOS yaongoza kitaifa katika taarifa ya utendaji wa SACCOS ya TCDC | URASACCOS