Habari zote

HAFLA

Tuzo nne kwa URA SACCOS kwenye kilele cha Siku ya Ushirika Duniani 2024, Tabora

Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko amekabidhi tuzo za chama bora cha ushirika wa kifedha, mtaji mkubwa daraja B, kurudisha kwa jamii na udhamini wa SUD 2024.

URASACCOS Admin

Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD) yamefikia kilele chake tarehe 6 Julai 2024 mkoani Tabora. Mgeni rasmi, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko, alitembelea mabanda ya maonesho likiwemo banda la URA SACCOS.

Mgeni rasmi alikabidhi tuzo, ambapo URA SACCOS imepata tuzo nne zilizopokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, CP Faustine C. Shilogile:

  • Tuzo ya chama bora cha ushirika wa kifedha (SACCOS)
  • Tuzo ya SACCOS yenye mtaji mkubwa, daraja B
  • Tuzo ya chama kilichorudisha zaidi kwa jamii
  • Tuzo kwa vyama wadhamini wa SUD 2024

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki: