HAFLA
Ni URA SACCOS tena: chama bora cha ushirika wa kifedha kwa mwaka wa tatu mfululizo
Kwenye kilele cha Siku ya Ushirika Duniani 2023 mjini Tabora, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amekabidhi tuzo kwa Mwenyekiti wa Bodi CP Benedict Wakulyamba.
URASACCOS Admin
URA SACCOS Ltd imeendelea kung’ara katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD), yaliyohitimishwa kitaifa Jumamosi tarehe 1 Julai 2023 mjini Tabora, kwa kupata tuzo ya Chama Bora cha Ushirika wa Kifedha nchini (SACCOS). Chama kimepata tuzo hii kwa mwaka wa tatu mfululizo kutokana na kufanya vizuri katika utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo inayosimamia vyama vya ushirika nchini.
Tuzo ilikabidhiwa na mgeni rasmi, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb), kwa Mwenyekiti wa Bodi ya URA SACCOS, CP Benedict M. Wakulyamba.
Vilevile chama kimepata tuzo miongoni mwa vyama vinavyoendelea kufanya vizuri katika uwekezaji wa Benki ya Ushirika, na tuzo ya nafasi ya tatu katika mabanda bora ya vyama vya kifedha.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

