MATUKIO
URA SACCOS yapokea ujumbe wa Ports SACCO kutoka Mombasa, Kenya
Wajumbe 20 wa bodi na wawakilishi wa Ports SACCO wamefika Makao Makuu kujifunza namna chama kinavyowafikia wanachama nchi nzima na kubadilishana uzoefu.
URASACCOS Admin
Tarehe 16 Aprili 2025 URA SACCOS Ltd imepokea ujumbe wa watu 20 kutoka nchini Kenya, wakiwa wajumbe wa bodi na wawakilishi wa Ports SACCO yenye makao makuu jijini Mombasa.
Ugeni huo umelakiwa na ACP Mussa A. Mussa, mjumbe wa bodi, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi, pamoja na Mtendaji Mkuu wa chama, ACP Kim O. Mwemfula.
Lengo la ujumbe huo lilikuwa kujifunza namna chama kinavyoweza kuhudumia na kuwafikia wanachama wake nchi nzima, kubadilishana uzoefu katika ushirika na kukuza ushirikiano. Ugeni huo umekuwa wenye manufaa makubwa ndani ya chama, ikiwa ni pamoja na kupata mbinu za kisasa za namna vyama vya ushirika vinavyojiendesha katika nchi jirani.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

