Habari zote

MATUKIO

URA Mobile yazinduliwa: huduma za chama kwenye simu saa 24

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jumanne Sagini amepongeza matumizi ya TEHAMA wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kidijitali wa URA SACCOS tarehe 30 Septemba 2023.

URASACCOS Admin

URA SACCOS Ltd imeendelea kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wanachama kwa kuzindua mfumo wa kidijitali ujulikanao kama URA Mobile, utakaowasaidia wanachama kupata huduma kupitia simu zao za mkononi saa 24.

Akizungumza tarehe 30 Septemba 2023 wakati wa hafla ya uzinduzi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (Mb), amekipongeza chama kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama ambao ni askari Polisi, watumishi raia wa Jeshi la Polisi na wenza wao, na kwa kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya TEHAMA ndani ya Jeshi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura, ameipongeza Bodi ya URA SACCOS kwa kuendesha chama kwa weledi, na kumpongeza IGP mstaafu Said Mwema kwa ubunifu wa kuanzisha chama hicho. Mwenyekiti wa Bodi, CP Benedict Wakulyamba, amesema hisa za chama zimefikia TZS bilioni 11.54 na idadi ya wanachama wanaokopa imeendelea kuongezeka.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki: