Habari zote

MATUKIO

URA SACCOS yakabidhi vifaa vya matangazo Shule ya Polisi Tanzania

DCP David Misime ameongoza makabidhiano ya vifaa vya kuboresha uwasilishaji wa mihadhara kwa wanafunzi wa TPS, kwa mujibu wa msingi wa saba wa ushirika.

URASACCOS Admin

Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya URA SACCOS, ameongoza makabidhiano ya vifaa vya matangazo (PA system) ili kuongeza ubora wa uwasilishaji wa mihadhara kwa wanafunzi wanaohudhuria mafunzo mbalimbali katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS).

Akizungumza na wakufunzi wa shule hiyo, DCP Misime alisema kitendo hicho kimefanyika kwa ajili ya kurudisha fadhila kwa jamii kwa mujibu wa msingi wa saba wa vyama vya ushirika. URA SACCOS, baada ya kuona uhitaji wa shule, ilinunua vifaa hivyo ili wanafunzi wafundishwe na kusikia vizuri, wakaenda kuwahudumia Watanzania kwa viwango vinavyotakiwa.

Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania, SACP Ramadhani Mungi, ametoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura, ambaye ni Mlezi wa URA SACCOS, na kwa uongozi mzima wa chama, na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo vifanye kazi iliyokusudiwa.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
URA SACCOS yakabidhi vifaa vya matangazo Shule ya Polisi Tanzania | URASACCOS