Habari zote
MIKUTANO
Vikao vya chama na wanachama: Ukonga, Kibiti, Arusha na Unguja
Watendaji wa URA SACCOS wamekutana na wanachama na wasio wanachama kukusanya maoni ya maboresho na kujibu hoja na maswali yao.
URASACCOS Admin
Watendaji wa URA SACCOS Ltd wameendesha vikao vya chama na wanachama pamoja na wasio wanachama katika maeneo mbalimbali mwanzoni mwa Septemba 2026. Vikao hivyo vililenga kukusanya maoni ya maboresho, kujibu hoja na maswali mbalimbali ya wadau hao.
Vikao vilifanyika katika maeneo yafuatayo:
- Viwanja vya Sitaki Shari, Ukonga, Dar es Salaam
- Wilaya ya kipolisi Kibiti, Pwani
- Viwanja vya FFU, Arusha
- Wilaya ya Mjini Unguja, Zanzibar
Maoni yaliyokusanywa yanasaidia chama kuboresha huduma zake na kuwafikia wanachama kote nchini.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

