Habari zote

MATUKIO

Nane Nane 2025: Waziri Mkuu apongeza ukuaji wa URA SACCOS hadi wanachama 51,331

Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea Kijiji cha Ushirika Dodoma na kupongeza chama kufikia mali zenye thamani ya TZS 162.4 bilioni. Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda naye alitembelea banda.

URASACCOS Admin

Maonesho ya Nane Nane kitaifa yaliendelea jijini Dodoma, ambapo tarehe 3 Agosti 2025 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, alitembelea Kijiji cha Ushirika kilichokuwa na banda la URA SACCOS.

Mhe. Majaliwa amepongeza chama kwa kukua hadi kufikia wanachama 51,331 na mali zenye thamani ya TZS 162.4 bilioni.

Tarehe 8 Agosti, Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Pinda naye alitembelea banda la URA SACCOS Ltd katika maonesho hayo na kujionea huduma zinazotolewa kwa wanachama.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki: