Habari zote

MATUKIO

Mwenyekiti wa Bodi Balozi CP Suzan Kaganda atembelea matawi ya Kigoma na Mwanza

Ziara ya kutembelea matawi na kukutana na wanachama imeongeza hamasa ya kuweka Akiba, Amana na Hisa na kubaini changamoto za matawi.

URASACCOS Admin

Mwenyekiti wa Bodi ya URA SACCOS Ltd, Balozi CP Suzan Kaganda, yupo kwenye ziara ya kutembelea matawi ya chama kuona namna yanavyotoa huduma kwa wanachama na kubaini changamoto zilizopo. Kupitia ziara hiyo amepata wasaa wa kuzungumza na wanachama na kuendelea kuwapa elimu ya ushirika, hususani uwekaji wa Akiba, Amana na Hisa pamoja na matumizi sahihi ya fedha.

Mkoani Kigoma ziara ilifanyika tarehe 23 na 24 Januari 2025, kwa kutembelea ofisi za tawi na kufanya kikao na wanachama. Tarehe 26 na 27 Januari alitembelea Tawi la Mwanza na kufanya kikao na wanachama wa mkoa huo.

Ziara hiyo imekuwa yenye manufaa makubwa kwa wanachama na chama, kwani imeongeza hamasa, tija na ari kwa watendaji na wanachama kuendelea kuongeza akiba zao na kukiamini chama. Mwenyekiti wa Bodi anaendelea na ziara katika matawi yote ya URA SACCOS Ltd.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
Mwenyekiti wa Bodi Balozi CP Suzan Kaganda atembelea matawi ya Kigoma na Mwanza | URASACCOS