Close

URA SACCOS LTD YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA DPA

Chama cha Ushirika wa akiba na mikopo cha Usalama wa Raia (URA SACCOS) Jumamosi 18/03/2023 kimekabidhi vifaa vya kufundishia katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA). Vifaa hivyo ni maalumu kwa kukuza sauti na kuboresha usikivu katika madarasa makubwa na mihadhara katika maeneo ya wazi (PA system). Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Uongozi wa Chama, Meneja mkuu msaidizi SSP Peter Mark Msuya ameeleza kuwa jambo hili limefanyika kwa kuzingatia Msingi wa saba wa ushirika unaovitaka vyama kurudisha sehemu ya faida kwa kuijali jamii hususani katika maeneo ya elimu, afya na maji. (Corporate social responsibility/CSR)
Naye Mkuu wa Chuo Dr SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa, Vifaa vilivyotolewa vitakuwa msaada mkubwa kwani kwa sasa chuo kina idadi kubwa ya wanafunzi katika mafunzo ya uongozi wa Polisi (uafisa na wakaguzi wasaidizi), Stashada na cheti. Vilevile ametaka salamu za pongezi zimwendee Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Camilius Wambura kwani ni jambo la kujivunia kupata msaada kutoka wadau wa ndani (URA SACCOS)
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya URA SACCOS Kamishna wa Polisi Benedict Michael Wakulyamba ambaye anaendelea na programu ya elimu katika mikoa na vikosi mbalimbali, amesema kwamba wao katika Bodi ya Chama wataendelea kuhakikisha chama kinaimarika huku kikifutata sheria, kanuni na miongozo ya ushirika kwani hiyo ndio silaha kuu ya kumuhakikishia mwanachama usalama wa fedha zake chamani.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *