Close

MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU WA KUMI NA TATU ULIOFANYIKA TAREHE 29-10-2021 MKOANI MBEYA

  1. KATIKA KUENDELEZA UTOAJI WA HUDUMA BORA YA MKOPO NA YENYE GHARAMA NAFUU KWA WANACHAMA, MKUTANO MKUU UMEAZIMIA KUPUNGUZA KIWANGO CHA RIBA YA MKOPO KUTOKA 8.1% KWA MWAKA NA KUWA 7.5% KWA MWAKA KUANZIA JANUARI 2022. PIA AKIBA NA AMANA ZITALIPWA RIBA YA 5.5% KWA MWAKA.
  2. ILI KUJENGA UELEWA WA PAMOJA WA CHAMA NA WELEDI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WANACHAMA, MKUTANO MKUU UMEAZIMIA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WATENDAJI, WAWAKILISHI NA WANACHAMA.
  3. KWA KUWA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA) NI NYENZO MUHIMU KATIKA UTOAJI HUDUMA BORA NA RAHISI KWA MWANACHAMA, MKUTANO MKUU UMEAZIMIA KUENDELEA KUKAMILISHA NA KUJIIMARISHA KATIKA MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHAMA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA MBALIMBALI ZA CHAMA.
  4. KUTOKANA NA UWEPO WA HAJA YA KUONGEZA MAPATO YA CHAMA, MKUTANO MKUU UMEAZIMIA KUWA BODI PAMOJA NA MENEJIMENTI WAKAFANYE UTAFITI WA KUWEZA KUPATA MAZAO MAPYA YA HUDUMA ILI KUPATA ONGEZEKO LA MAPATO KATIKA CHAMA KWA MFANO TOTO AKIBA, WAKALA WA BIMA n.k.
  5. KWA LENGO LA KUONGEZA IDADI YA WANACHAMA, MKUTANO MKUU UMEAZIMIA KUJIKITA KATIKA KUWAFIKIA WASIO WANACHAMA NA KUWAPATIA ELIMU YA KINA KUHUSU FAIDA ZA KUWA WANACHAMA PAMOJA NA FURSA WANAZOZIKOSA KWA KUTOKUWA WANACHAMA.
  6. KWA LENGO LA KUKUZA MTAJI WA CHAMA, MKUTANO MKUU UMEAZIMIA MWAKA 2022 UWE MWAKA WA UHAMASISHAJI MKUBWA WA KUONGEZA VIWANGO VYA UCHANGIAJI WA AKIBA, AMANA NA HISA ILI TATHMINI ITAKAPOFANYIKA KATIKA MKUTANO MKUU UJAO MAAMUZI YA KUONGEZA MUDA WA MAREJESHO YA MKOPO YAWEZE KUFANYIKA.
  7. KUTOKANA NA FAIDA NDOGO INAYOPATIKANA KATIKA UWEKEZAJI WA CHAMA KATIKA HISA ZA NMB NA VODACOM, MKUTANO MKUU UMEAZIMIA HISA HIZO ZIUZWE NA FEDHA HIZO ZIPELEKWE KWENYE MIKOPO YA WANACHAMA ILI KUIMARISHA HUDUMA YA UTOAJI WA MIKOPO AMBAYO NDIO RASILIMALI KUU YA CHAMA.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *