Habari na matukio
Taarifa kwa wanachama, hafla, mikutano mikuu na matukio ya ushirika.
5MATUKIO
URA SACCOS yapokea ujumbe wa Ports SACCO kutoka Mombasa, Kenya
Wajumbe 20 wa bodi na wawakilishi wa Ports SACCO wamefika Makao Makuu kujifunza namna chama kinavyowafikia wanachama nchi nzima na kubadilishana uzoefu.
5MATUKIO
Mwenyekiti wa Bodi Balozi CP Suzan Kaganda atembelea matawi ya Kigoma na Mwanza
Ziara ya kutembelea matawi na kukutana na wanachama imeongeza hamasa ya kuweka Akiba, Amana na Hisa na kubaini changamoto za matawi.
6MIKUTANO
Mkutano Mkuu wa 16 wafanyika Mwanza chini ya kaulimbiu "Wekeza kwa Maendeleo Endelevu"
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mhe. Ally Gugu, amepongeza chama kwa tuzo na hati safi mfululizo mbele ya wawakilishi na watendaji zaidi ya 200.
4MATUKIO
URA SACCOS yashiriki maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo (ICUD 2024)
Kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mbugani, Mwanza, banda la URA SACCOS limetembelewa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege.
4MIKUTANO
URA SACCOS yashiriki mafunzo na mkutano wa ACCOSCA nchini Kenya
Mkutano wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika umefanyika Naivasha ukishirikisha nchi 44, Tanzania ikiwakilishwa na wajumbe wapatao 70.
2HAFLA
URA SACCOS yajinyakulia tuzo ya SACCOS bora mahali pa kazi
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Zubery Omella, amekabidhi tuzo ya TCDC kwa Meneja Mkuu ACP Kim O. Mwemfula kwenye uzinduzi wa taarifa ya utendaji wa SACCOS 2023.
5TAARIFA
URA SACCOS yaingia makubaliano na ALAF: mabati kwa bei nafuu kwa wanachama
Kupitia makubaliano yaliyosainiwa tarehe 3 Septemba 2024, wanachama wanaweza kupata mabati bora ya ALAF kwa bei rafiki kupitia chama chao.
4MATUKIO
Elimu ya ushirika kwa askari wa mafunzo ya awali, Shule ya Polisi Moshi
Mjumbe wa Bodi DCP David Misime na watendaji wa chama wamewaandaa vijana hao kuwa wanachama wa URA SACCOS kupitia elimu ya fedha ya siku tatu.
5MIKUTANO
Bodi na menejimenti wapata mafunzo Nairobi na kuahidi kuboresha huduma kwa wateja
Ziara ya mafunzo kwa Kenya National Police DT SACCO imelenga kuongeza weledi katika kuwainua kiuchumi watumishi wa Jeshi la Polisi na familia zao.
